Serikali inatarajia kupeleka milioni 100 mwezi Agosti katika kijiji cha Mahege na Ruaruke wilayani Kibiti mkoani Pwani ,ili kuanza mradi wa ujenzi wa maji ambao utagharimu milioni 735.7 hadi kukamilika kwake.   

Naibu Waziri wa Maji , Mhandisi Maryprisca Mahundi  amesema kuwa wanakijiji hao watarajie kuondokana na kero ya ukosefu wa maji safi na salama ,ambapo amewahakikishia kuwa kero hiyo inakwenda kubaki historia.   

Ameyasema hayo ,wakati wa ziara yake  ya kikazi , wilayani Kibiti ambapo ametembelea kijiji Cha Mahege kuzungumza na wananchi na miradi ya maji Nyamisati, Ruaruke na mradi wa maji wa Miwaga.    

Aidha Naibu Waziri Mahundi ,amemugiza Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Ahmed, kutatua changamoto ya kuzungusha maji kwa kutumia dizeli na kuhakikisha anashugulikia tatizo kwa kwenda TANESCO ili uendeshaji ubadilike.

Sambamba na hayo Naibu Waziri Mahundi amemuagiza meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA )Kibiti, Pascal Kibanjulo, kuangalia namna ya kuongeza vituo vya maji vitano huko Ruaruke ili kusogeza huduma ya upatikanaji wa maji kwa wakazi

Hata hivyo amesema kuwa serikali inatekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya kutatua changamoto ya ukosefu wa maji mijini na vijijini ,hivyo wanaendelea kupeleka fedha katika miradi mbalimbali ikiwemo miradi viporo iliyofika hatua nzuri ya ujenzi kwa asilimia 70-90 . 

Balo la Lwanga lawaneemesha wachezaji Simba SC
Jakaya Kikwete mwenyekiti mpya GPE