Waziri wa mambo ya ndani ya nchi George Simbachawene amesema Januari hii ndiyo mwisho wa tatizo la uhaba wa vitambulisho vya Taifa (NIDA), litakapopatiwa ufumbuzi na kuanza kutolewa kwa wingi.

Kwa mujibu wa Gazeti la Mwananchi kiongozi huyo amesema kilichochelewesha kufikia hatua hiyo mapema ni mchakato wa manunuzi ndani ya serikali ambao ulikuwa na vipengele vingi.

Simbachawene amesema mashine hiyo hainunuliwi ikiwa imefungwa pamoja, bali kila sehemu ya utendaji kazi ndani yake inakuwa na mkataba wake na itafungwa kati ya Januari 20 hadi 25, 2021.

Gazeti hilo lilifanya mahojiano hayo kutokana na ukweli kwamba watu wengi waliojiandikisha wamekuwa hawapati vitambulisho kwa muda na badala yake wanapewa tu namba, huku katika baadhi ya maeneo hata namba zenyewe zikiwa hazijatolewa.

“Mashine nayo inafanya kazi kizamani sana, kumbuka tunazalisha vitambulisho 2000 kwa siku kiasi ambacho ni kidogo ukilinganisha na idadi ya watanzania waliotambuliwa , lazima tubadilike,”amesema Simbachawene.

Kwa mujibu wa Simbachawene idadi ya Watanzania waliokuwa wametambuliwa hadi mwishoni mwa mwaka 2020 walikuwa Milioni 18.5, lakini waliopewa vitambulisho walikuwa Milioni 6.3 tu na kwamba Wwtu Milioni 12.2 walikuwa hawajavipata.

Afisa Mkuu Georgia asema Trump ni muongo
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Januari 5, 2021