Shirikisho la soka dunaini FIFA, limetangaza ratiba ya michuano ya klabu bingwa duniani ambayo inadhaminiwa na Alibaba E-Auto na kufanyika nchini Japan kuanzia Disemba 8 hadi 18.

Michuano hiyo itashirikisha klabu sita kutoka katika mabara yote sambamba na klabu mwenyeji.

Michezo ya michuano hiyo itachezwa katika viwanja viwili vya Suita City Football Stadium (mjini Osaka) na International Stadium Yokohama (mjini Yokohama).

Hadi sasa Klabu 3 zimeshathibitika kushiriki michuano hiyo ambazo ni Real Madrid (Mabingwa wa Ulaya) waliotwaa Ubingwa wao Mwezi Mei, na Timu nyingine ni Club America ya Mexico pamoja na mabingwa wa bara la Oceanic ambao wailitwaa Ubingwa wao Mwezi Aprili, Auckland City FC.

Afrika inatarajia kuwakilishwa na bingwa wa michuano ya klabu bingwa barani humoa mbayo itafikia tamati mwezi Oktoba mwaka huu.

Juan Jesus Gonzalez Aendelea Kupeta Azam FC
Paul Makonda Amjibu Meya wa Dar es salaam