Mamlaka ya usimamizi wa wanayamapori Tanzania (TAWA), imechangia kiasi cha Shilingi Milioni 10 kuitikia wito wa Rais Samia Suluhu Hassan, wa kuzisaidia timu za Serengeti Girls na Tembo Warriors ambazo zinapaswa kushiriki michuano ya kimataifa huko India na Uturuki.

Uchangiaji wa fedha hizo, uliongozwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa katika kikao maalumu kilicho fanyika jijini Dar es salaam ambacho kimewashirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo ya michezo kwa lengo la kujadili na kuchangia timu hizo.

Mamlaka hiyo ya usimamizi wa wanyama pori imechangia fedha hizo kupitia kwa Afisa Mahusiano wake, Vicky Kamata kwa niaba ya Kamishna wa uhifadhi ambaye amesema wameamua kuunga mkono juhudi la Raisi katika kuendeleza michezo nchini.

Kiasi hicho cha pesa, kitasaidia kuwapa motisha timu zote mbili za wanawake wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Girls), na timu ya wenye ulemavu (Tembo Warriors), kujiandaa vyema kwa ajili ya mashindano ya kimataifa.

Jumla ya fedha zilizopatikana katika kikao hicho ni shilingi Billioni 1.26, ambazo zitawawezesha kuelekea nchini Uingereza katika jiji la Southampton kwa ajili ya maandalizi ya michuano hiyo.

Magonjwa yasiyopewa kipaumbele kudhibitiwa
Young Africans: Dawa ya Azam FC inachemka