Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania – TAWA, imepokea meli nyingine ya Kimataifa iliyobeba watalii kutoka nchini Ufaransa.

Meli hiyo ya utalii ijulikanayo kama Le Jacques – Cartier Ponant, imewasili Machi 9, 2023, iikiwa imebeba watalii 125 watakaotembelea Hifadhi ya Urithi wa Utamaduni wa Dunia Magofu ya Kilwa Kisiwani.

Meli ya kitalii ya Le Jacques – Cartier Ponant.

Sehemu nyingine watakazotembele Watalii hao, ni Songo Mnara na wakiwa hapo watafanya utalii wa Malikale na fukwe.

Hata hivyo, Meli hiyo ya kitalii ya Le Jacques – Cartier Ponant, inaendelea na safari katika visiwa vya Pemba na Unguja, na zifuatazo ni picha zikionesha baadhi ya matukio mara baada ya kuwasili kwa Watalii hao.

Sixtus Mapunda ndani, Nyamsenda nje Ukuu wa Wilaya
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Machi 10, 2023