Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Fatma Abubakar Mwasa leo Agosti 20, 2022, ametembelea banda la TAWA katika viwanja vya Gymkhana Mkoani Morogoro, ambako Mbio za riadha za ‘Selous Marathon’ zimefanyika.

Akiwa katika banda hilo la TAWA, Mwasa aliweza kupata maelezo mafupi kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na TAWA.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Fatma Abubakar Mwasa, akiongoza Marathon katika Viwanja vya Gymkhana Mkoani humo.

TAWA imetumia mbio riadha za ‘Selous Marathon’ kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana katika Pori la Akiba la Selous, lililopo mikoa ya Lindi na Pwani,

Eneo jingine la Pori la akiba la Selous ni Pori la Akiba la Pande lililopo jijini Dar es Salaam na Pori la Akiba la Wamimbiki, lililopo Mkoani Morogoro.

Serikali kuwakopesha Wavuvi Boti za Kisasa
Samia awapatia wavuvi Vijana Bil. 33