Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro, imepata ugeni toka Mamlaka ya Uhifadhi Wanyamapori Tanzania (TAWA), ikiongozwa na Kaimu Kamishna wa Uhifadhi, Mabula Nyanda uliofika ofisini kwake kwa ajili ya kumsalimia, kujitambulisha na kumpa taarifa zinazohusu Uhifadhi katika Mkoa wa Morogoro.

Katika salamu hizo, Kamishna wa Uhifadhi alimpatia taarifa ya shughuli mbalimbali Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Fatma Mwasa ambazo TAWA inazishughulikia hasa katika eneo la Pori Tengefu la Kilombero, Fursa, changamoto na hatua mbali mbali ambazo TAWA imeshachukua katika kukabiliana nazo.

Ugeni wa TAWA uluiofika Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Fatma Mwasa.

Akiukaribisha ugeni huo, na mara baada ya kupokea taarifa hizo Mkuu huyo wa Mkoa ameishukuru TAWA kwa kufika ofisini kwake, kumkaribisha Morogoro, na kuonyesha ushirikiano katika masuala mbalimbali yanayohusu Maendeleo ya Mkoa.

Mwasa, ameelezea umuhimu wa TAWA kwa mkoa wa Morogoro katika masuala ya Uhifadhi wa Vyanzo vya maji ambavyo vimekua vikiharibiwa kutokana na uvamizi wa mifugo, ukataji miti hovyo na uchomaji wa misitu.

TAWA katika Picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Fatma Mwasa (wa tano kutoka kushoto).

Amesema, “Uwepo wenu hapa mkoa wa Morogoro ni muhimu sana hasa ikizingatia watu zaidi ya milioni 11 wa Mkoa wa Morogoro na maeneo jirani wanategemea maji ambayo vyanzo vyake ni kutoka katika mkoa wa Morogoro.

Aidha, ameongeza kuwa atashangaa ikiwa TAWA wataharakisha kuhamia Dodoma wakati bado mkoa wa Morogoro unawahitaji katika katika kufanukisha masuala ya uhifadhi na kulinda vyanzo vya maji ambavyo bila jitihada za dhati huenda vitakauka.

Meck Mexime mtumaini kibao Kampala-Uganda
Kisinda afunguka kilichomrusha Young Africans