Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA), limefuta matokeo yote ya Watahiniwa 2194, ambao ni sawa na asilimia 0.16 ya Watahiniwa 1,350,881 waliofanya Mtihani.

Taarifa hiyo imetolewa hii leo Desemba mosi, 2022 wakati NECTA ikitatangaza matokeo ya Darasa la saba kwa mwaka 2022 na kusema ilibaini wanafunzi hao kufanya udanganyifu katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi.

Wanafunzi wakiangalia matokeo kwenye ubao.

Kaimu Katibu Mtendaji wa NECTA, Athumani Almasi akitangaza matokeo hayo amesema Watahiniwa zaidi ya milioni 1.07 kati ya Milioni 1.34 ambao ni sawa na asilimia 79.62 wamefaulu kwa kupata madaraja A,B na C.

Mtihani huo, wa Darasa la saba uliofanyika Oktoba 5-6, 2022 umeonesha uwepo wa upungufu wa ufaulu kwa asilimia 2.35 ingawa idadi ya watahiniwa waliofaulu imeongezeka na kufikia 165,600 sawa na asilimia 18.24.

Kutazama matokeo yote ya darasa la saba kwa mwaka huu 2022 bonyeza hapa https://necta.go.tz/psle2022/psle.htm

NECTA yavifungia vituo 24 vya Mitihani
Rais Samia aongoza maadhimisho siku ya Ukimwi