Rais Samia Suluhu Hassan hii Leo tarehe 3 Mei 2022 ameshereheka sikukuu ya Eid El Fitri katika matukio matte tofauti na yakifanyika jijini Dar es Salaam na Jijini Arusha.

Mapema asubuhi Rais Samia alishiriki Swala ya Eid El Fitri katika Msikiti Mkuu wa BAKWATA Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa anatoka katika Msikiti Mkuu wa BAKWATA uliopo Kinondoni Muslim mara baada ya kushiriki Swala ya Eid El Fitri pamoja na Waumini wengine wa dini ya Kiislamu Jijini Dar es Salaam tarehe 3 Mei, 2022.

Baada ya kushiriki Swala ya Eid jijini Dar es Salaam, Rais Samia Suluhu Hassan alisafiri mpaka jijini Arusha na kuhutubia katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliofanyika Jijini Arusha.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia Wadau mbalimbali wa Sekta ya Habari katika Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari yaliofanyika Jijini Arusha tarehe 03 Mei, 2022.

Hata hivyo baada ya kumaliza kuhutubia jijini Arusha, Rais Samia Suluhu Hassan jioni ya Leo amehutubia katika Baraza la Eid El-Fitr jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia Baraza la Eid El-Fitr  lililoandaliwa na Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) katika ukumbi wa Mikutano wa  Julius Nyerere Conventional Centre Jijini Dar es Salaam  tarehe 03 Mei, 2022. 
Viongozi wa Afrika watakiwa kushirikian na vyombo vya habari
Rais Samia atoa maelekezo sheria za habari