Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), imeshindwa kuweka wazi suala la kuendelea kuidhamini klabu ya Simba, mara baada ya mkataba wa sasa utakapofiklia kikomo baadae mwaka huu.

Kampuni hiyo imekua ikiidhamini klabu ya Simba pamoja na Young Africans kwa miaka kadhaa sasa, lakini siku za hivi karibu pameibuka tetesi kuhusu mustakabali wa udhamini huo.

Tayari Young Africans wameshaonyesha kwa vitendo kuchana na udhamini wa TBL kwa kuvaa jezi ambazo hazina nembo ya bia la Kilimanjaro katika michuano ya kimataifa ambayo wanaenedelea kushiriki hivi sasa.

Young Africans wamekua wakivaa jezi zenye maandishi ya Quality Center kifuani, kampuni ambayo ipo chini ya mwenyekiti wao Yusuf Manji.

Kwa mantiki hiyo, udhamini wa TBL ulionekana kusalia kwa upande wa klabu ya Simba pekee ambayo msimu ujao itashiriki michuano ya ligi kuu ya soka Tanzania bara pamoja na kombe la shirikisho (FA CUP).

Alipoulizwa Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, Pamela Kikuli kuhusu ukweli wa jambo hilo, alisisitiza kuwa kampuni yao haipo katika nafasi ya kulisemea suala hilo kwa sasa.

“Ninasema TBL kwa sasa hatuko kwenye nafasi ya kuzungumzia suala hilo kama tutaendelea kuidhamini Simba au la, wakati ukifika tutazungumza,” amesema meneja.

VIDEO: SAUTI ZETU WITH BERTHA PETER
Valencia CF Yamuweka Sokoni Shkodran Mustafi