Shirika la Viwango Tanzania (TBS), na TradeMark East Africa (TMEA), wametia saini za makubaliano ya ufadhili yenye thamani ya bilioni 9, kwa lengo la kuimarisha utekelezaji wa viwango na usimamizi wa ubora wa bidhaa.

Akizungumza na waandishi wa Habari kataika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Dkt. Athuman Ngenya amesema msaada huo ni muhimu kwa uchumi wa nchi na shughuli zote za uendeshaji, ambazo ziliimarisha ufanisi wa utoaji wa huduma kwa jumuiya ya wafanyabiashara na kukuza upatanishi wa viwango vya kikanda.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango (TBS), Dkt.Athuman Ngenya na Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA) Monica Hangi 

Amesema, “TBS inapenda kuishukuru TMEA kwa juhudi kubwa na msaada mkubwa unaotolewa ili kuongeza ufanisi katika usimamizi na utekelezaji wa viwango vyote viwili, vya hiari na vya lazima (Kanuni za Kiufundi), kwa lengo la kuwezesha biashara.”

Naye, Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA), Bi. Monica Hangi amesema juhudi za kurahisisha biashara zimewekwa ili kukabiliana na changamoto hizo, sambamba na kupunguza vikwazo vya kibiashara na visivyo vya Ushuru nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango (TBS), Dkt.Athuman Ngenya na Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya TradeMark East Africa (TMEA) Monica Hangi 

Amesema, hatua za awali za Mifumo ya Kusaidia iliyolenga kukuza biashara kupitia uboreshaji wa Viwango na mifumo ya SPS nchini Tanzania, inasalia kuwa kipaumbele cha TradeMark East Africa.

Aidha, amesema TBS imekuwa mmoja wa washirika wakuu ambao wameonyesha uwezo wa kutoa matokeo yanayoonekana katika miradi mbalimbali inayoungwa mkono na TMEA. Hivyo ametoa wito wa kuendelea kushirikiana katika kuhakikisha kuwa awamu hii ya mradi pia inaenda kuwa na mafanikio makubwa.

Waziri Mkuu awasilisha salamu za Rais Samia Japan
Mhandisi wa Maji apewa siku 30 kukamilisha kazi