SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS), limesema huduma zote ambazo zimekuwa zikitolewa Makao Makuu au katika ofisi zao za kanda sasa zinapatikana katika banda lao la maonesho ya sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja hivyo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari hii leo Julai 03, 2022 Afisa Uhusiano TBS, Bi. Neema Mtemvu amesema maonesho hayo yamewakutanisha wadau pamoja na wananchi ili kupata huduma mbalimbali na kuweza kutatua changamoto wanazokutana nazo.

Mmoja wa mafisa wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), akitoa maelezo kwa wananchi walaiofika kutembelea banda hilo ili kufahamu mambo mbalimbali katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Uwanja wa Mwalimu Nyerere Sabasaba Jijini Dar es Salaam.

“Kuna wale ambao wanahitaji kufahamu masuala ya Viwango, wanafika hapa tunamuelezea ni namna gani ambavyo ana umuhimu wa kushiriki katika mchakato wa kuandaa viwango na vilevile kama anataka kiwango ni namna gani anakipata na hapahapa tunaweza kumuwezesha,” amesema Bi. Neema.

Aidha ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wafanyabiashara, wenye viwanda pamoja na wananchi kutembelea banda la TBS katika maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Uwanja wa Mwalimu Nyerere Sabasaba Jijini Dar es Salaam.

Maafisa Viwango na Wataalamu mbalimbali wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) wakiwa na utayari wa kutoa huduma katika Maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kwenye Uwanja wa Mwalimu Nyerere Sabasaba Jijini Dar es Salaam.
Ruto nusura kumpiga kofi Rais Uhuru
Mchungaji awateka nyara waumini 'awalamba kisogo' ni unyakuo