Shirika la Viwango TBS limewatoa hofu wananchi kutokana na hali ya sintofahamu ya kuhusiana na juice ya Ceres ya Afrika Kusini inayotokana na tundala apple kuwa na sumu Kuvu ambapo imesema kuwa juice hizo hazijaingia Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 16, 2021 Mkurugenzi wa udhibiti ubora kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Lazaro Msasalaga Amesema kuwa kimsingi taarifa inayoenea mtandaoni ni taarifa ya awali ya mzalishaji kuitoa endapo bidhaa aliyoisambaza kwa wateja wake inahitilafu yoyote, ambapo taarifa hiyo hutumwa kupitia mtandao wa kimataifa wa mamlaka ya uthibiti usalama wa chakula ulio na nchi wananchama 186.

Amesema kuwa Tanzania ni Moja ya wananchama lakini mzigo ulionekana kuwa na sumu Kuvu hiyo Tanzania haijaingia, huku akielezea kuwa kwa kulihakikisha hilo TBS ilimtembelea Wakala wa juice hiyo Tanzania kukagua mzigo na kukuta mzigo wenye hitilafu za kiusalama wa kuanzia Toleo la Juni 14-30, 2021 Tanzania haikusambaziwa Bali ni nchi za Kenya,Jamhuri ya Congo, Zimbabwe na nyinginezo.

Hata hivyo Mkurugenzi wa udhibiti ubora TBS, Lazaro amesema mzigo utakaoingia nchi wa hilo Toleo utateketezwa kwa mujibu wa sheria.

Young Africans yaenda Songea
Serikali yatenga Bilioni 45 kutekeleza anwani za makazi nchini