Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limekukanusha uvumi uliokuwa umeenea kuhusiana na uwepo wa maji aina ya Dew yanayodaiwa kutengenezwa nchini na kusababisha vifo kwa watumiaji nchini Nigeria.

TBS wamesema kuwa kwa zaidi ya mwezi sasa wakaguzi wao wamekuwa wakitafuta maji hayo katika masoko ya ndani bila ya mafanikio na kuwasiliana na Bodi za Viwango ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Kusini mwa Bara la Afrika (SADC) mbazo zimehakikishia kuwa hakuna na maji hayo katika nchi zao.

Hivyo, TBS imehakikishia umma kuwa taarifa hizo sio za kweli isipokuwa ni uzushi na uongo kwani hakuna maji yoyote ya aina ya Dew yanayotengenezwa nchini Tanzania.

Pia wametoa rai kwa watumiaji wa bidhaa kutoka Tanzania kudharau taarifa hizo, kwani zinalenga kuharibu biashara za kimataifa kwa Tanzania pamoja na kuharibu sifa za nchi ya Tanzania,” imeeleza taarifa hiyo ya TBS.

Mzunguuko Wa Tano Waunguruma Ulaya
#HapoKale