Shirika la viwango Tanzania (TBS) imeandaa mafunzo kwa wadau wa vipuri vya magari pamoja na karakana hapa nchini lenye lengo la kuwaanda washiriki kuwa wenye mwelekeo mzuri zaidi na wa kiuweledi katika kutekeleza matakwa ya viwango husika.

Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo leo Jijjini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Dkt.Athuman Ngenya amesema watumiaji hutegemea waagizaji na wauzaji wa vipuri vya magari na wenye karakana ili wawashauri juu ya aina na ubora wa vipuri sahihi kwa magari yao.

“Ikiwa mtumiaji hawezi kupata vipuri vyenye ubora na sahihi kwa mahitaji ya gari lake, hii inasababisha kuwepo kwa malalamiko juu ya thamani ya maisha yao na fedha zao”. Amesema Dkt.Ngenya.

Amesema yapo baadhi ya magari baada ya kukaguliwa na kupimwa yanagundulika kuwa na kasoro mbalimbali, hivyo hutakiwa kufanyiwa marekebisho kabla ya kuruhusiwa kutumika hapa nchini.

“Wahusika wanatakiwa kufanya marekebisho kwenye karakana zenu, hivyo ni jukumu la Shiriika  kuhakikisha wadau wote kwenye sekta hii wanajua viwango vinavyopaswa kuzingatiwa katiika kutoa huduma hiyo”. Amesema.

Aidha amewataka wadau hao kutumia fursa hiyo ukizingatia nchi inaendeleza miradi ya kimkakati ikiwemo uchimbaji wa gesi, ambapo itafikia wakati ambapo watakaofanikiwa kutoa huduma katika miradii  hiyo ni zile karakana zilizothibitisha mifumo yao kulingana na viiwango husika.

Amesema Shirika linaunga mkono juhudi zote zinazofanywa na Serikali ili kuhakikisha kuwa bidhaa zinazoingizwa hapa nchiini zinakidhi matakwa ya ubora ikiwemo vipuri vya magari na karakana zinazotumia vipuri hivyo ili biashara iiwe inafanywa katika mifumo inayotolewa.

Sigara Inaua watu Milioni 8 Kila mwaka: Prof Janabi
Rais Samia arejea kutoka Glasgow Scotland.