Shirika la Viwango Tanzania (TBS), limewataka wazalishaji na waingizaji wa bidhaa kushirikiana na taasisi za serikali katika kuhakikisha kuwa ubora wa bidhaa zinazozalishwa na kuingizwa nchini unazingatiwa ili kusaidia katika kulinda uchumi wa nchi na kupunguza hasara kwa wafanyabiashara.

Hayo yamesemwa na Mkaguzi kutoka kitengo cha Bidhaa zinazotoka nje ya nchi (TBS), Andalalisye Mwakyonde wakati akizungumza na waandishi wa habari waliofanya ziara katika Makao  Makuu ya TBS Ubungo  Jijini Dar es Salaam.

Mwakyonde amesema kuwa TBS inafanya ukaguzi mipakani na Bandarini ili kuhakikisha kuwa bidhaa zote zinakidhi usalama na ubora uliowekwa hivyo amewataka waingizaji wa bidhaa kufuata taratibu zote pindi wanapotaka kuingiza bidhaa nchini.

Afisa Usalama wa Chakula Mkuu TBS, Bi. Coletha Sarimbo akizungumza na waandishi wa habari ambao wamefanya ziara katika Makao  Makuu ya TBS Ubungo leo Jijini Dar es Salaam.

“Shirika la Viwango Tanzania lina kampuni tano zinazofanya ukaguzikatika maeneo ya uzalishaji mkubwa wa bidhaa zinazoingizwa nchini ikiwa ni pamoja na CCIC Intertek , Bureau Veritas, SGS pamoja na TUV walioanza shughuli za ukaguzi mapema Agosti mwaka huu”. Amesema Mwakyonde

Naye, Afisa Usalama wa Chakula Mkuu TBS, Coletha Sarimbo amesisitiza umuhimu wa usajili wa bidhaa hususani za chakula na vipodozi katika kuhakikisha ubora na usalama wa bidhaa husika ili kulinda afya za watumiaji na kusaidia wananchi kupata taarifa sahihi ya bidhaa kulingana na viambata vilivyopo kwenye bidhaa hizo.

Aidha ametoa wito kwa wafanyabiashara wanaoandaa matangazo yanayohusu vyakula na vipodozi kuyawasilisha TBS kwa ajili ya mapitio na baadae kupewa kibali ili kuhakikisha matangazo hayo hayamrubuni mlaji.

Young Africans yaihofia Mbeya City, Kaze afunguka
Van Gaal: Tupo hapa kucheza soka, hatugombani