Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza kuwachukulia hatua kali watu wote wanaotumia majina na taarifa za uongo kwenye mitandao ya kijamii.

Hayo yamesemwa jana na Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo, James Kilaba alifanya mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuzindua kampeni maalum ya kutoa elimu juu ya matumizi sahihi ya mitandao ya kijamii.

Mamlaka hiyo imeanzisha kampeni itakayojulikana kama ‘Darasa Mtandao’ ambayo itatangazwa pia kupitia vituo vya runinga, radio na magazeti kwa lengo la kuongeza ufahamu na elimu zaidi kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii.

Tumeamua kuzindua kampeni hii ili kuwasaidia wananchi kuepuka makosa ya kimtandao na kuepuka kufanyiwa utapeli au wizi mitandaoni kwa sababu matukio mengi ambayo yamekuwa yakiripotiwa au kulalamikiwa yanazuilika kwa watu kupewa elimu ya matumizi sahihi ya mitandao,” alisema Kilaba.

Alisema kuwa pamoja na mambo mengine, kupitia kampeni hiyo watasaidia kuwaelimisha wananchi kuepuka utapeli na wizi wa mitandaoni ikiwa ni pamoja na namna ya kutunza ‘password’ zao na taarifa nyingine muhimu.

Emmanuel Mbasha azungumzia uwezekano wa kurudiana na Flora
Tundu Lissu apangua hoja za kumng’oa Bulaya Kortini kwa saa mbili