Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA, Dkt. Jabiri Bakari amesema wataendelea kuwawezesha wabunifu chipukizi wa TEHAMA, ili kufanya majaribio ya ubunifu wao kwa kutoa bure rasilimali za mawasiliano kwa kipindi cha miezi mitatu.

Dkt. Jabiri Bakari ameyasema hayo kwenye mjadala unaohusisha Usalama Mtandaoni, uliondaliwa na jukwaa la Kimataifa la Usalama Mtandaoni (Global Cybersecurity Forum), hii leo Novemba 10, 2022 nchini Saudi Arabia.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA, Dkt. Jabiri Bakari (wa pili kutoka kushoto), akiwa katika mjadala unaohusisha Usalama Mtandaoni nchini Saudu Arabia.

Oktoba 7, 2022 Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari alisema Serikali kupitia Wizara ya Habari imesema itahakikisha wabunifu kwenye sekta ya TEHAMA, wanachangia uchumi wa nchi yao kwa kuongeza ajira kwa vijana.

Kupitia mkutano uliowashirikisha, wabunifu kwenye sekta ya TEHAMA uliolenga kuona namna bora ya kuzisaidia kampuni hizo za ubunifu kuweza kufanya biashara, Katibu Mkuu huyo alisema, sekta ya mawasiliano nchini ina fursa kubwa ya kuweza kuongoza kwenye ukanda wa nchi za Afrika Mashariki na kati kwenye soko la ajira.

Majaliwa ataka tafiti zaidi kubaini vyanzo vya maji
Waihoji Serikali kuisaidia DRC wakati nchi ina uhitaji