Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, James Kilaba amesema vifurushi vilivyokuwa vinatumika awali vinaweza kutumia hadi siku nne kurejea.

Kilaba amesema hata walipofanya mabadiliko ya bei zilizotakiwa kutumika, Kampuni za Mawasiano zilipewa muda wa kufanya mabadiliko, hivyo hata kuvirudisha inachukua muda.

TCRA ilisitisha matumizi ya bei mpya za data Aprili 2, baada ya wananchi kulalamikia kupanda kwa bei za vifurushi vya data.

Breaking: Rais Samia ateua Makatibu Wakuu wa Wizara, Manaibu, Wakuu wa Taasisi za Serikali
Hospitali ya Taifa Muhimbili yatoa ufafanuzi kufuatia ujumbe wa Kigwangala