Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza adhabu yake dhidi ya kituo cha runinga cha Clouds TV kutokana na kurusha kipindi cha Take One kilichomhoji shoga maarufu jijini Dar es Salaam wiki chache zilizopita.

TCRA imekitaja kipindi hicho kuwa kilikuwa na mlengo wa upotoshaji na kinyume cha maadilihivyo kuitaka Clouds TV kuwaomba radhi Watanzania kwa siku tano mfululizo.

Take One

“Clouds Television inatakiwa kuwaomba radhi watazamaji wake na Watanzania kwa ujumla kutokana na kuwakwaza pamoja na kuwasababishia usumbufu kwa kurusha mada inayoongelea ushoga kwa namna ya upotoshaji kupitia kipindi cha Take One kulishorushwa tarehe 28 Juni 2016,” imesema taarifa ya Kamati ya Maadili na Maudhui ya TCRA.

“Taarifa ya kuomba radhi itoke siku tano mfululizo, kwenye taarifa zao za habari za saa moja na nusu usiku, na saa tano usiku kuanzia siku ya kusomwa hukumu ili na uthibitisho wa taarifa hizo uletwe Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania siku ya Jumatano tarehe 13 mwezi wa 7 mwaka 2016 kabla ya saa kumi jioni,” imeongeza.

Kipindi hicho cha Take One kinachoongozwa na mtangazaji, Zamaradi Mketema kilizua mgogoro mkubwa na kukosolewa vikali na Watanzania walioitaka Serikali kuichukulia hatua kali Clouds TV.

Baada ya kutolewa adhabu hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Ruge Mtahaba amesema kuwa matendo ya ushoga ni lazima yapingwe na kukemewa bila kunong’ona.

“Hakuna namna ya kuwa mbishi na kuingia kwenye vita ya vitu vidogo vidogo, na kama kukemea unakemea bila kunong’ona,” Ruge anakaririwa.

Video: Taarifa ya mfumuko wa bei wa Taifa 2016
Foleni kubwa ya magari yaua watu 15