Mamlaka ya kudhibiti Mawasiliano nchini, TCRA imeongeza muda wa usijili kwa wamiliki wa vyombo vya habari mtandaoni (Blogu, majukwaa, Redio au Televisheni) ambao bado hawajapata leseni ya utoaji huduma hiyo kuwa tayari wawe wamekamilisha usajili huo mpaka ifikiapo Juni, 30, 2018.

TCRA imesema ifikapo tarehe hiyo wale ambao bado watakuwa hawana leseni watatakiwa kuondoa hewani mitandao yao na kuendelea kuwasilisha maombi ya usajili wakiwa hawapo hewani.

Ameongezea kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa kwa atakayeenda kinyume na agizo hilo.

Taarifa hiyo ni kufuatia agizo lililotolewa Juni 11, 2018 ambapo TCRA ilitoa siku 5 kwa wamiliki na watoa maudhui mtandaoni kuwa tayari wameshafanya usajili na kuwa na leseni ya kutoa huduma hiyo kwa mujibu wa sheria ya mtandaoni.

Hivyo jana Juni 15, 2018 ilikuwa mwisho wa kutekeleza agizo hilo, aidha taarifa hiyo imebainisha ongezeko la muda kwa wamiliki wa vyombo vya habari mtandaoni ili kukamilisha zoezi hilo la usajili na umiliki wa leseni.

TRA yataifisha mali za thamani ya shil. mil 3
Ommy Dimpoz anusurika kifo, 'nimefanyiwa oparesheni'