Kuanzia Leo Juni 11, 2018 Mamlaka ya Kudhibiti Mawasiliano nchini, TCRA imepiga marufuku kwa vyombo vya habari kupitia maudhui ya mtandaoni ambavyo havina leseni ya kuendesha shughuli hiyo kuweka jambo au taarifa yeyote katika mitandao yao.

TCRA imetoa siku 5 kuanzia leo Juni 11, hadi Juni 15, 2018 kuhakikisha vyombo hivyo vya habari vinakamilisha usajili na kuwa na leseni ya urushaji wa matangazo kupitia mtandao, imesisitiza kuwa kuanzia Juni 15, mwaka huu hatua kali zitachukuliwa kwa watakaokiuka agizo hilo.

Kufuatia agizo hilo Uongozi wa Mtandao wa Jamii Forums uliojikita katika kuhabarisha umma mtandaoni umeomba radhi kwa usumbufu utakaojitokeza mara baada ya kuamua kutii agizo hilo la kusitisha huduma ya utoaji habari mpaka pale utakapokamilisha usajili huo.

Katika ukurasa wake wa Facebook umeandika hivi;

”Kutokana na notisi iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Juni 10, 2018 inayotoa muda mfupi wa kututaka kusitisha utoaji huduma mara moja kabla ya Juni 11, 2018, tunalazimika kutii mamlaka na hivyo huduma hii haitapatikana kwa muda wakati tukifanya jitihada za kuhakikisha huduma inarejea.

Tunasikitika kuwa tunalazimika kufikia hatua hii ghafla lakini ni matumaini yetu kuwa wateja wetu mtaendelea kuwa wavumilivu katika kipindi hiki” Umesema Uongozi wa JamiiForums.

Aidha TCRA inaendelea kuutahadharisha umma kwa mujibu wa kanuni ya 18 ya maudhui ya mtandaoni (Blogu, majukwaa mtandaoni, redio na televisheni mtandaoni) bila kuwa na leseni.

Serikali kuchakachua sheria ya Uzazi na Afya, wanaume nao watajwa kunufaika
SSRA yatoa sharti zito kwa wanachama Mifuko ya Hifadhi ya Jamii