Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imewatoa hofu wanafunzi waliohitimu katika vyuo vilivyozuiwa hivi karibuni kufanya udahili, huku ikikanusha taarifa za kuvifungia udahili wa kozi tofauti vyuo 22 zilizozagaa.
Hivi karibuni TCU ilitangaza kusimamisha kufanya udahili  vyuo vitano baadhi vikiwamo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo Kikuu cha Mtakatifu Francis cha Ifakara Morogoro, Chuo cha Mtakatifu Joseph cha Dar es Salaam na Chuo cha IMTU cha Dar es Salaam vyote kwa kozi ya udaktari.
Hayo yamesemwa na Kaimu Katibu Mtendaji wa TCU, Eliuther Mwageni alipokuwa akifanya mahojiano na mwandishi wa Dar24 kuhusu kufungiwa kwa vyuo hivyo ni kwa muda mpaka vitakapokamilisha vigezo vinavyotakiwa.
“Kuna vigezo vinavyotakiwa kufikiwa ili chuo kiweze kusajiliwa  na hivi vyuo hatujavifungia ila tumevisimamisha kwa muda mpaka vikidhi vigezo vyetu”Alisema Mwageni.
Aidha kuhusu taarifa za vyuo 22 kusimamishwa kudahili wanafunzi katika kozi mbalimbali zilizozagaa kwenye mitandao, Mwageni alisema taarifa hizo ni za uzushi, zina lengo la kupotosha jamii hivyo hazina ukweli wowote.

Serengeti Boys Kuweka Kambi Madagascar
Waziri Mhagama Azindua Ripoti Ya Utafiti Wa Next Generation