Akicheza mechi yake ya kwanza msimu wa 2015/2016, Lionel Messi hakuhitaji dakika nyingi kuwanyamazisha mashabiki duniani kote.
Nyota huyo mwenye miaka 28, raia wa Argentina alifunga magoli mawili kwa mipira miwili iliyokufa ‘Free Kick’ Barcelona ikishinda 5-4 dhidi ya Sevilla katika mechi ya fainali ya Uefa Super Cup iliyopigwa jana.
Magoli hayo yaliyopishana kwa dakika 9 tu yaliufanya mtandao wa Twitter uwe ‘busy’ kupita maelezo.
Mshindi huyo mara nne wa Ballon d’Or, katika maisha yake ya soka hajawahi kufunga free kick mbili ndani ya mechi moja.
Kwa kiwango alichoonesha nyota huyo kijana wa Barcelona, ana uwezekano mkubwa wa kushinda tuzo binafsi ya tano ya Ballon d’Or mwezi Januari mwakani.
Tumekukusanyia baadhi ya Tweets baada ya Messi kuandika historia ya aina yake.

 

 

 

 

 

 

 

Mbowe Azungumzia Afya Yake Akiwa Muhimbili
Ndoa Mpya Ya TFF Na Vodacom Kufungwa Leo