Sekretarieti ya ajira nchini imejipanga kupunguza changamoto za malalamiko ya  baadhi ya waombaji wa fursa  za ajira kwa kuanzisha mifumo miwili mipya ya kielektroniki  ambayo itawafikia waombaji wengi zaidi na kwa haraka.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es saalam Kaimu Naibu Katibu Tehama Ndg, Mtage Ugullum amesema sababu za kuanzisha mfumo huo ni  kuepuka  kuchukua muda mrefu kukamilisha mchakato wa uombaji fursa za ajira , utunzaji wa kumbukumbu za waombaji, gharama  za uendeshaji wa mchakato  pia kupanua wigo hususani vijijini.

Hata hivyo amesema mafanikio ya utumiaji wa mifumo hii mipya yameonekana  ambapo uendeshaji wa mchakato wa ajira  umepungua kutoka siku 90 mpaka 52 na  waombaji wa kazi kuwa na uhakika wa kupokelewa kwa maombi hayo tofauti na hapo mwanzo.

Aidha Bi,Ugullum amesema mtumiaji yoyote wa simu atakayekuwa amejisajili kwenye  mfumo atakuwa na uwezo wakupata taarifa  za papo kwa hapo kama kuna nafasi mpya za ajira zimetangazwa.

DSC_0815 - Copy

Sanjari na hayo ametaja mfumo unaojulikana kama ‘recruitment portal’ unapatikana kwa anuani ya portal.ajira.go.tz na mfumo wa pili ni kwa ajili ya kupata ujumbe mfupi wa fursa za ajira  kupitia simu ya mkononi ‘job alert system’ kwa kubofya *152*00#.

Pamoja na hayo sekretarieti ya Ajira  imewataka wahitimu wa vyuo mbalimbali  kujiunga na mfumo wa TEHAMA wa kuombea ajira kwani ndio njia ya pekee inayotumika kupokelea maombi ya michakato yote inayoendeshwa na sekretarieti ya Ajira.

Hadi kufikia 29 mei 2016 jumla ya waombaji wa fursa za ajira waliojiandikisha kwenye mfumo wa utumaji wa maombi ya kazi walikuwa ni 97,765.

 

 

Wanafunzi wa UDSM wagoma, Bodi ya Mkopo yakwamisha ahadi ya Magufuli
Twiga Stars Kupimana Ubavu Na Rwanda