Mtu mmoja amekamatwa baada ya mawasiliano yake kupitia mtandao wa Telegram kuonesha akiwasiliana na kundi la kigaidi linalojiita Dola la Kiislamu akiomba dola 190,000 kununulia magari  kwaajili ya kufanyia mashambulizi.

Mtu huyo mwenye umri wa miaka 38 alihamia Ujerumani mwaka 2014 na amekamatwa katika mji wa Saarbrucken uliopo mpakani mwa Ufaransa, baada ya mtoa taarifa wa polisi kuchati naye kwa mtandao wa Telegram.

Mshukiwa huyo amekiri kuwasiliana na wapiganaji wa IS, lakini amekanusha mashitaka ya kupanga mashambulizi ya kigaidi.

Tayari mshukiwa huyo alishaomba euro 180,000 ambazo angeweza kuzitumia kununua na kutengeneza magari aliyodhamiria kuyajaza mabomu kabla ya kuyaendesha kwenye mikusanyiko ya watu, wamesema maafisa wa upelelezi.

Azam FC Yakusanya Point Tatu Zanzibar
TTCL Kudhamini Mashindano Ya Soka la Ufukweni