Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, Hussein Ruhava amekiri kuwepo kwa sintofahamu juu ya uwepo wa mtu anayefahamika kwa jina la ‘Teleza’ ambaye amedaiwa kuwaingilia kimwili wanawake wasiokuwa na waume usiku kwenye wilaya hiyo bila ridhaa yao.

Kwa mujibu wa Meya huyo, amesema kuwa malalamiko juu ya uwepo wa ‘Teleza’ yalifika kwenye Baraza la Madiwani ambapo waliagiza Jeshi la Polisi kulishughulikia suala hilo.

Aidha, Meya Ruhava amesema tukio hilo halina uhusiano wowote na imani za kishirikina bali vilikuwa ni vitendo vya kiuhalifu.

“Ni kweli mwanzoni mwa mwaka huu tulipokea taarifa ya kuingiliwa kwa wanawake bila ridhaa yao, lilitufikia kwenye vikao vya Baraza la Madiwani na tuliamuagiza OCD (Mkuu wa Polisi Wilaya) ayafanyie kazi na walijitahidi kulizima hilo zoezi.” amesema Meya Ruhava

 

Hata hivyo, wiki iliyopita kupitia Mkuu wa wilaya ya Kigoma Mjini Samson Anga alieleza kutolitambua suala hilo

RC Hapi amkalia kooni aliyemzushia kulazwa makaburini
Breaking: Mourinho atimuliwa Man United