Msajili Mstaafu wa Vyama vya Siasa Nchini John Tendwa, amesema kuwa  kuanzishwa kwa vyama vingi hapa nchini  kuchangiwa na Vuguvugu kutoka kwa jamii  ambalo liliungwa mkono na mabadiliko ya kisiasa ulimwenguni baada ya kuanguka kwa dola za kisoshalisti.

Amesema anguko hilo lilifanya jumuiya za ulaya mashariki kuingia kwenye mfumo wa vyama vingi baadaye kusambaa duniani kote.

Aidha, Tendwa amesema kuwa mfumo wa vyama vingi hapa nchini ulianza baada ya Serikali kuunda Tume iliyoratibu maoni ya Watanzania ambayo iliongozwa na Marehemu Jaji Francis Nyalali, ambapo ripoti hiyo ilionyesha asilimia 20 tu walikubali mageuzi na asilimia 80 walipendekeza kubaki na mfumo wa chama kimoja.

“Serikali ilianza kufuata maoni ya wananchi wachache kuhusu mfumo wa vyama vingi hatua ambayo ilikuwa ni uamuzi wa busara kwani ndani ya mfumo huo, kuna ushindani wa kifikra, mawazo na sera na taratibu mbadala wa kuongoza nchi kwa misingi ya kidemokrasia yenye kuheshimu utu na kulinda haki za binadamu”amesema Tendwa.

Hata hivyo amesema kuwa Tanzania ina vyama vya siasa vyenye Usajili wa kudumu 19 na chama kimoja kina usajli wa muda.

Amevitaja baadhi ya vyama hivyo ni pamoja na Chama cha Mapinduzi (CCM), Chama cha Wananchi (CUF), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tanzania Labour Party(TLP), NCCR-mageuzi, ACT-Wazalendo na Tadea.

Serikali yatenga sh. bil.15 kutoa mafunzo kwa vijana zaidi 2,500
Mbarawa: TCRA tokomezeni wizi mtandaoni