Tetemeko kubwa la Ardhi limetokea Kusini mwa Taiwan na kuangusha jengo la ghorofa 17 ambapo taarifa za awali kutoka nchini humo zimeeleza kuwa watu wanne wamepoteza maisha.

Jopo la waokoaji lilifanikiwa kuwatoa ndani ya jengo hilo watu 200 katika kipindi cha muda mfupi tangu kuanguka kwa jengo hilo, na uokoaji ulikuwa unaendelea.

Meya wa mji wa Tainan aliwaambia waandishi wa habari kuwa mtoto mchanga alikuwa miongoni mwa watu wanne waliofariki. Alisema kuwa takribani watu 30 hawajapatikana lakini wanaamini wako hai ila wamenasa kwenye jengo hilo.

Meya huyo alieleza kuwa juhudi za kuwaokoa watu hao zinaendelea.

Tetemeko hilo limetajwa kuwa na kipimo cha Ritcher 6.4 kutoka katika mji wa Tainan.

Kufuatia tetemeko hilokubwa, kumetokea matetemeko mengine madogo matano ndani ya nchi hiyo.

Polisi wafariki kwenye Msafara wa Rais Magufuli
KIKWETE: Tulikubali kurudiwa uchaguzi wa Zanzibar kwa shingo upande