Tetesi zinasena nahodha wa Aston Villa Jack Grealish, 24, atapewa mkataba mpya wa pauni 100,000 kwa juma baada ya Manchester United kuonesha haina nia ya kutaka kumsajili.

Manchester City bado hawajawasiliana na FC Barcelona kuhusu beki wa kulia Sergi Roberto, licha ya kuhusishwa kwa kiasi kikuwa na mchezaji wa kimataifa wa Uhispania, 28, na haina mpango huo.

  • Mabingwa wa Ligi ya England (EPL) Liverpool wanakaribia kumaliza mkataba wa pauni milioni 9 kwa mlinzi wa Aissa Mandi wa Real Betis na Algeria mwenye urmi wa miaka 28.
  • Liverpool pia wanajitayarisha kwa dau la pauni milioni 10 kwa beki wa kushoto wa Norwich na Ireland Kaskazini Jamal Lewis, 22, wakati wanatafuta nani wa kuvaa viatu vya Andy Robertson.
  • Kiungo wa kati wa Southampton raia wa Denmark Pierre-Emile Hojbjerg, 24, amepangiwa kujiunga na Tottenham kwa pauni milioni 15, huku beki wa Uingereza Kyle Walker-Peters, 23, akipata mkataba wa kudumu wa pauni milioni 12.
  • Klabu za Liverpool, Crystal Palace na Wolves zimeonyesha nia ya kumsajili winga wa Senegal, 22, Ismaila Sarr kutoka Watford iliyoshushwa daraja.
  • Leicester City wamefanya mazungumzo na FC Barcelona kuuliza ikiwa inaweza kumchukua mshambuliaji wa Ureno, 20, Francisco Trincao kwa misimu miwili ya mkopo, ikiwemo wajibu wa kumnunua kwa pauni milioni 45 (€50m) mwisho wa msimu.
  • Aliyekuwa kiungo wa kati wa Manchester United Angel Gomes, 19, amejiunga na klabu ya Ufaransa ya Lille kwa mkataba wa miaka mitano baada ya kuondoka Old Trafford msimu huu.
  • Aliyekuwa beki ya kulia wa Chelsea Branislav Ivanovic amesema kuna uwezekano akawasiliana na aliyekuwa kocha wake Carlo Ancelotti akiwa Everton.
  • Klabu ya Southampton imeonesha nia ya kumsajili mlinzi wa Groningen, Deyovaisio Zeefuik, 22, lakini mholanzi huyo anaaminika anapendelea kuhamia Ujerumani.
  • Mshambuliaji wa Queens Park Rangers Eberechi Eze, 22, anamezewa mate na mahasimu wao wa London Crystal Palace na West Ham, huku klabu hiyo inayoshiriki Ligi ya Mabingwa ikiweka thamani ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Under-21 kuwa pauni milioni 20.
  • Klabu ya Newcastle United inammezea mate mshambuliaji wa Bournemouth raia wa Norway Josh King, 28, na kiungo wa kati wa Welsh David Brooks, 23, baada ya Cherries kushushwa daraja.

Michuano ya kimataifa kumpeleka Kichuya Namungo FC
Magufuli kuchukua Fomu wiki hii