Matajiri wa klabu bingwa Ufaransa Paris St-Germain wamepanga kumsajili mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford, 22, na raia wa England kwenye majira ya kiangazi ya usajili.

Mshambuliaji kutoka Brazil Neymar, 28, anahitaji kurudi Catalunya FC Barcelona licha ya matajiri wa Jiji la Paris kuonyesha nia ya kuendelea kumtumia staa huyo ambaye amebakiza miaka miwili kwenye kandarasi yake.

  • Manchester United watapoteza kiasi cha pauni milioni 25 kutoka kwa mdhamini wao wa vifaa vya michezo Adidas endapo watashindwa kufuzu kucheza michuano ya Ulaya msimu ujao.
  • FC Barcelona wameimpa ofa Arsenal na Newcastle United juu ya kumpata winga wa Kibrazil Philippe Coutinho, 28, ili kupata pesa ya usajili wa straika wa Argentina na Inter Milan Lautaro Martinez, 22.
  • Beki wa kushoto wa Liverpool Andrew Robertson, 26, anategemea kuingia mkataba mpya na mabingwa wapya wa Ligi Kuu nchini England Liverpool ambao unaweza ukawa wa muda mrefu zaidi.
  • Chelsea yaiwinda saini ya kipa wa Atletico Madrid Oblak, Man United kukosa pesa ndefu wasipofuzu kucheza Ulaya. Chelsea wako tayari kutoa Euro milioni 100 kwa ajili ya kumnasa mlinda mlango wa Atletico Madrid na timu ya taifa ya Solvenia Jan Oblak, 27.
Wassira achukua fomu Bunda, Lugola arudi Mwibara
Makonda ajitosa Kigamboni, Msukuma, Kanyasu warudi Geita