Serikali kupitia Wizara ya Afya, imesema inachakata taarifa kuhusu tetesi za uwepo wa mlipuko mpya wa Uviko – 19 nchini na kuwataka Wananchi kuondoa hofu.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ambaye amesema Wizara ya Afya inachakata taarifa hizo zilizokusanywa kutoka Hospitali na Vituo mbalimbali ndani ya wiki hii kisha itatoa taarifa endapo lipo ongezeko la magonjwa ya mfumo wa hewa.

Amesema, “kwa taarifa za Wagonjwa waliopimwa virusi vya covid-19 wiki ya kuanzia Mei 6 – 12, 2023 watu sita kati ya 288 walithibitishwa kuwa na corona idadi ambayo ni pungufu ikilinganishwa na wiki ya Aprili 29 – May 5, 2023 na  hakuna kifo chochote cha covid kilichothibitishwa.”

Aidha, Waziri Ummy ameongeza kuwa, Wizara inaendelea kufuatilia kwa karibu Hospitali mbalimbali na itatoa taarifa kamili, na kuwaomba Wananchi kuendelea kuzingatia kanuni za afya.

Waliopanga kumpindua Rais watupwa Gerezani
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Mei 15, 2023