Joto la tetesi za kuwepo uhusiano wa mapenzi kati ya wakali wa muziki wa Nigeria, Wizkid na Tiwa Savage, limemuamsha mume wa zamani wa mwimbaji huyo, Tee Billz.

Tee Billz ambaye pia alikuwa meneja wa Tiwa ametumia mtandao wa Instagram kueleza imani yake kwa mkewe huyo wa zamani pamoja na mkali wa Soco.

Amesema anaamini kuwa Tiwa hawezi kumkosea heshima kiasi hicho kwani anajua Wizkid ni mdogo wake na hivyo hawawezi kuchanganya damu kwa mtindo huo.

Kupitia ujumbe huo mrefu uliokuwa na maneno mengi yenye ukakasi pia, Tee Billz amemshukuru Wizkid pia akidai kwa muda wote wamekuwa ndugu ambao anaamini tetesi kama hizo haziwezi kuwa kweli na kwamba hata baba zao kwenye muziki kama Don Jazzy hawawezi kuruhusu hilo litokee.

“Ninasema hili hadharani kwa watu wote wanaokuja kwangu na habari zisizo za heshima!!! Kwa taarifa yenu, asante Titi kwa kwa kuniheshimu! Maoni yenu kuhusu yeye na mdogo wangu Wizzy ni upuuzi. Don Jazzy hawezi kuruhusu hilo. Tiwa atembee na Wiz? Hataruhusu hilo,” Tee ameandika.

Ameenda mbali na kupendekeza kuwa kama Tiwa atataka kutoka na watu maarufu basi viwango vyake ni vya kutoka na mtu kama Aliko Dangote ambaye ni tajiri namba moja Afrika, Mr. Adeleke aka Baba Olowo na wengine.

Amewapongeza Wiz na Tiwa kwa muunganiko wao kimuziki na kuwataka waendelee kutoa vitu vikali kwa ajili ya mashabiki wao.

Kadhalika, amempongeza Wiz Kid kwa dili alilopata la kampuni ya Nike kutoa jezi zake, ambazo zimefanikiwa kuisha ndani ya dakika 10 zilipoingia sokoni.

Tiwa na Wiz Kid wamekuwa karibu na kufanya muziki mzuri. Moja kati ya nyimbo zilizofanya vizuri ni ‘Ma Lo’ ambayo Tiwa alimpa shavu Wizkid Ayo.

Video: Tazama mwili wa Kofi Annan ulivyopokelewa kwa heshima
Ivan Rakitic: Luka Modric mchezaji bora wa dunia

Comments

comments