Kocha Mkuu wa Man United, Ole Gunnar Solskjaer anahofia kwamba hatma ya kazi yake itakuwa haijulikani iwapo timu yake itashindwa kwa mabao mengi ugenini dhidi ya Liverpool.

Kwamujibu wa vyombo vya habari nchini Uingereza baadhi ya wachezaji wamepoteza matumaini na raia huyo wa Norway, yeye anaamini baadhi yao wamekataa kumsikiliza.

Mchezaji wa zamani Lee Shape amebainisha kuwa Solskjaer anahitaji kitita cha £300m kutumia katika dirisha lijalo la uhamisho na kumnunua mshambuliaji wa Tottenhama na England Harry Kane (26).

Katika hatua nyingine, Chelsea na mshambuliaji wa Marekani Christian Pulisic, 21, amekiri kukasirishwa kwa kukosa muda wa kucheza zaidi tangu uhamisho wake wa £58m kutoka Borussia Dortmund. (Guardian).

Huku gazeti la the standard lime mnukuu mkufunzi Roy Hodgson aliyesema kuwa klabu Crystal Palace italazimika kumsaini mshambuliaji mpya mwezi januari iwapo wanataka kumaliza katika orodha ya timu sita za kwanza katika jedwali na pia analenga kuwasajili mabeki wawili wapya wakati dirisha la uhamisho litakapofunguliwa.

Kane anafaa kuondoka Tottenham na badala yake kuhamia Manchester City, kulingana na beki wa zamani wa England Glen Johnson.

Huku Liverpool huenda ikapokea kitita cha £4.5milioni kati ya kile cha £84milioni wanazowadai Barcelona baada ya kumnunua kiungo Philippe Coutinho, 27, ambaye alihamia Nou Camp mwaka 2018. (Mirror).

klabu ya Everton inafikiria kumnunua mchezaji anayelengwa na Manchester United, Moussa Dembele katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari. Mshambuliaji huyo wa Ufaransa , mwenye umri wa miaka 23 anaweza kugharimu £40m kutoka Lyon.

Mshambulaji wa Arsenal Gabriel Martinelli, 18, anakabiliwa na chaguo katika hatma yake ya kimataifa kwa kuwa anahitajika na Italia pamoja na Brazil. Alizaliwa nchini Brazil lakini lakini babake ni raia wa Italia hivyo basi anaweza kuwakilisha timu zote mbili.

Tetesi kutoka Newcastle Chronicle, zinaeleza kuwa Mshambuliaji wa Venezuela Salomon Rondon(30) amekiri kwamba angependelea kusaini mkataba wa kudumu na klabu ya Newcastle lakini hakupatiwa fursa kubadili uhamisho wake wa mkopo wa msimu uliopita kuwa kandarasi ya kudumu na hivyo basi ameenda kujiunga katika klabu ya China ya Dalian Yifang.

Kocha Rwanda ampumzisha Kagere
Baba aua mtoto kwa kula chakula walichobakiza kwenye sherehe