Leicester City wameacha mpango wao wa uhamisho kwa ajili ya kiungo wa kati wa Inter Milan Christian Eriksen, 28, kwa sababu mchezaji huyo wa kimataifa wa Denmark anataka mshahara wa 300,000 pauni kwa wiki. (Telegraph)

Bayern Munich wamethibitisha haja yao ya kusaini mkataba na Mlinzi wa RB Leipzig Mfaransa Dayot Upamecano, mwenye umri wa miaka 22 ambaye katika mkataba wake ana kipengele cha kumuachia cha thamani ya pauni 40 milioni (Mirror)

Manchester United, Manchester City na Chelsea kwa pamoja wameonyesha nia yao katika ya kumtaka Dayot Upamecano, ambaye mkataba wake hautasainiwa hadi msimu ujao. (Goal)

Licha ya klabu mbali mbali kuonyesha kumtaka kiungo wa kati wa Real Madrid Martin Odegaard mwanye umri wa miaka 22, anakaribia kabisa kukamilisha uhamisho wake wa mkopo kuelekea Arsenal. (Sport – in Spanish)

Arsenal wanataka kusaini mkataba na kiungo wa kushoto Kieran Tierney, 23, kabla ya kumalizika kwa dirisha la uhamisho wa wachezaji mwezi Januari. (Express)

West Ham huenda wakashusha bei yao wanayoitaka kwa kiungo wa kati wa Declan Rice, 22, hadi kufikia pauni 50 milioni kwa sababu ya athari za janga la virusi vya corona. (90min)

Kiungo wa kati wa Tottenham na England Dele Alli, 24, amemuomba mwenyekiti Daniel Levy asimuwekee pingamizi katika uwezekano wake wa kuhamia Paris St-Germain. (90min)

Hammers wanajiandaa kuboresha dau la pauni 16milioni kwa ajili mshambuliaji Mnorway wa Bournemouth Joshua King, 29. (Sun)

Hata hivyo, Burnley wamejiunga na West Ham na West Brom katika kinyang’anyiro cha kusaini mkataba na King, ambaye mkataba wake unakamilika msimu huu. (Sky Sports)

Kiungo wa kati wa Ecuador Moises Caicedo, 19, anatarajiwa kusafiri kuelekea England Ijumaa kukamilisha mkataba wa pauni 4.5milioni wa kuhamia Brighton kutoka klabu ya Independiente del Valle. (Sky Sports)

IGP Sirro ajitambulisha rasmi
Simba SC uso kwa macho na TP Mazembe, Kocha mpya bado