Bosi wa Manchester City Pep Guardiola anafikiria kumsajili beki wa kushoto wa Bayern Munich na Austria David Alaba, 28, kwenye dirisha kubwa la usajili.

  • Wakala wa kiungo mshambuliaji wa Manchester City Kevin de Bruyne, 29, amesema mchezaji huyo raia wa Ubeligiji hataondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu hata kama timu hiyo itapigwa rungu ya kutoshiriki michuano ya Uefa.
  • Arsenal wanataka kumbakiza kipa namba mbili Emiliano Martinez, 27, ambaye ameonyesha kiwango bora sana tangu alipoumia kipa namba moja Beno.
  • Mbweha Leicester City wanafikiria uwezekano wa kumpata mshambuliaji wa Real Madrid Jovic ambaye amekosa nafasi ya kucheza kunako klabu hiyo yenye mataji mengi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
  • Mkurugenzi wa michezo wa Borussia Dortmund Michael Zorc amesema wameanza kufikiria atakayekuwa mubadala wa Jadon Sancho, 20, ambaye amepanga kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu, Manchester United na Real Madrid zimekuwa zikihusishwa kumhitaji winga huyo. Na
  • Kiungo wa Jamhuri wa watu wa Ireland Jeff Hendrick, 28, amepanga kufanya uhamisho wa kushitukiza wa kwenda kujiunga na AC Milan akitokea Burnley.
  • Real Madrid imepanga kuwanunua mastaa wawili wanaosakata kabumbu kwenye ligi ya Ufaransa Kylian Mbappe wa Paris St Germain na Eduardo Camavinga, 17, wa Rennes, Madrid imewaambia wasiingie mikataba mipya kunako klabu yake mwaka 2021.
Mashabiki 30,000 kushuhudia Simba SC Vs Young Africans
FA waomba radhi kuchemsha kwa VAR