• Thomas Partey wa Atletico Madrid, 27, anataka sana kuhamia Arsenal lakini The Gunners inahitajika kuwaacha baadhi ya wachezaji wao kuondoka kwanza kabla ya kutimiza kigezo cha kumsajili kiungo huyo wa kati raia wa Ghana anayesemekana kwamba thamani yake ni pauni milioni 44.5.
 • Chelsea imesema thamani ya N’Golo Kante ni pauni milioni 80 huku Inter Milan ikionesha nia ya kumsajili kiungo huyo wa kati wa Ufaransa, 29.
 • Hata hivo, mchezaji huyo aliyekuwa Leicester Kante hana mpango wa kuondoka Chelsea.
 • Kocha wa Tottenham Jose Mourinho yuko tayari kumuuza kiungo wa kati wa Ufaransa Tanguy Ndombele, 23 ambaye usajili wake uliweka historia.
 • Tottenham imemtangaza aliyekuwa mwenyekiti wa Swansea Trevor Birch kuwa mkurugenzi wao mpya wa masuala ya soka.
 • Newcastle inajaribu kufikia makubaliano ya Callum Wilson, 28, wa Bournemouth ambayo yatamuwezesha winga wa Scotland Matt Ritchie kujiunga na Cherries, lakini Aston Villa pia inamnyatia mshambuliaji huyo wa England.
 • Klabu bingwa nchini Ufaransa Paris St-Germain imeahidi kutoa pauni milioni 25 pamoja na pauni milioni 5 za ziada kwa beki wa kulia wa Arsenal Hector Bellerin, huku Bayern Munich na Juventus pia zikionesha nia ya musajili mlinzi huyo wa Uhispania, 25.
 • PSG imewasiliana na winga wa Inter na Slovakia Milan Skriniar, 25, ambaye pia Tottenham inammezea mate.Crystal Palace imekataa ofa ya pauni milioni 20 kwa ajili ya mshambuliaji wa Norway Alexander Sorloth, 24, kutoka RB Leipzig.
 • Leicester imekubali kufikia makubaliano ya pauni milioni 22 kumsajili beki Mbeligiji Timothy Castagne, 24, kutoka Atalanta.
 • AS Monaco inamnyatia kiungo wa kati wa Watford Abdoulaye Doucoure baada ya Everton kushindwa kuafikiana kwa dau linalohitajika kumsajili.
 • Juventus inataka kumsajili mshambuliaji wa Barcelona na Uruguay Luis Suarez, 33, au wa Roma, Bosnia Edin Dzeko, 34.
 • Mlinda lango Kepa Arrizabalaga, 25, yuko tayari kusalia Chelsea na kuendelea kupigania nafasi yake, hata ikiwa klabu hiyo itafanikiwa kumsajili mlinda lango mpya.
 • Al Nassr imetoa ofa ya euro milioni 20 kwa mchezaji wa Arsenal raia wa Ujerumani Mesut Ozil, 31, sawa na pauni milioni 18 katika mkataba wa kujiunga na klabu hiyo ya Saudi Arabian.
Matumaini mapya ugojnwa wa utapiamlo Tanzania
Nana: Sina mahusiano na yeyote, zaidi ya....