Mshambuliaji wa Crystal Palace na timu ya taifa ya Ivory Coast Wilfried Zaha, 27, anavutiwa kujiunga na matajiri wa Jiji la Ufaransa Paris Saint Germain.

  • Southampton wamepanga kuanza mazungumzo ya kimkataba na mlinzi wao wa kushoto Ryan Bertrand, 30, ambapo anahusishwa kwenda kwa mbweha Leicester City.
  • Kiungo mshambuliaji wa Bournemouth Ryan Fraser, 26, amekusudia kutoingia kwenye mkataba mpya na klabu yake hivyo anaweza akaondoka bure mwishoni mwa msimu huu.
  • Manchester United watacheza michezo miwili ya kirafiki siku ya Ijumaa dhidi ya West Brom katika dimba la Old Trafford ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kurudi kwa ligi ya EPL.
  • Kiungo mshambuliaji wa Villarreal Santi Cazorla, 35, amesema ameshafanya maamuzi juu ya hatima yake licha ya kusema hata weke wazi kwa sasa maamuzi hayo, mchezaji huyo wa zamani wa Arsenal atakuwa nje ya mkataba majira ya kiangazi.
  • Mkurugenzi wa Real Madrid amesitisha mpango wa kucheza mechi sita za nyumbani katika dimba la Wanda Metropolitano uwanja wa wapinzani wa jadi Atletico Madrid. Dimba Santiago Bernabeu liko katika ukarabati mkubwa.

Msamaha wa Magufuli kwa zimamoto watoka na onyo kali
Kocha Sven awatumia salamu Ruvu Shooting