Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wakuu wa Wilaya wapya 37, kuwahamisha vituo vya kazi Wakuu wa Wilaya 48 huku wengine 55 wakibakia katika vituo vyao vya kazi.

Katika Wakuu hao wapya wa Wilaya, aliyekuwa Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilosa iliyopo Mkoani Morogoro, huku Mwanahabari, Grace Kingalame akiteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale.

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Godwin Gondwe sasa anaenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma, huku Nicki Simon akihamishiwa Wilaya ya Kibaha kutoka Wilaya ya Kisarawe alikokuwa akihudumu awali.

Aliyewapiga Wanafunzi asimamishwa kazi
Zaidi ya watu 1,000 wafariki kwa Kipindupindu