Katika kuonyesha kuunga mkono  juhudi  za rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.John Joseph Magufuli,mamlaka ya  chakula na dawa nchini wametoa hundi ya shilingi milioni 17.7 kwaajiri ya madawati 236.

Hundi hiyo imetolewa na mkurugenzi wa TFDA bw,Hiiti Sillo mapema hii leo katika Ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Bw Sillo alisema pamoja na majukumu yake ya msingi TFDA inao utaratibu wa  kuithamini jamii na  kuisaidia katika shughuli mbalimbali.

Aidha aliongeza kuwa  hii ni mara ya pili kwa mamlaka hiyo kutoa  mchango wa madawati katika shule mbalimbali ambapo mwaka 2013 TFDA ilitoa jumla ya madawati 100 kwa shule za msingi zilizopo mabibo.

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ameshukuru msaada huo na kuzikumbusha taasisi zingine za serikali kuiga mfano wa TFDA wa kutoa misaada ambayo itaendeleza mahusiano mazuri na jamii.

Hata hivyo Makonda aliongeza kuwa bila elimu nchi haiwezi kuwa na watalaam wanaokizi viwango hivyo wadau na taasisi mbalimbali kusaidia sekta hiyo ya elimu na kukuza ushirikiano.

Video: Makonda apokea Milioni 31.7 za Madawati DSM
TRA Yazindua Zoezi La Uhakiki,Uboreshaji Taarifa Za Mlipa Kodi