Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imesema inafanya uchunguzi kwa wanaofanya biashara haramu kupitia mitandaoni wakisambaza picha ya Dawa inayodaiwa kuuzwa kwa bei rahisi na kutumika kuongeza maumbile ya binadamu huku dawa hiyo ikiwa maalumu kwa matumizi ya kuongeza vitamini kwa wanyama.

Mkurugenzi wa TFDA, Adam Fimbo amesema kitendo hicho ni kosa la jinai na tayari wameanza mchakato wa kufanya msako wa watu hao kwani dawa hizo zinazosambazwa na kuuzwa zinamadhara mengi kwa binadamu.

Ameongezea kuwa madhara hayo hutegemea na aina ya kemikali zilizowekwa ndani ya dawa hizo.

”Hii iliyosambazwa mtandaoni ni ya vitamini ingawa vitamini kiuhalisia haina madhara lakini dawa hii imewekwa maalumu kwa matumizi ya wanyama na si binadamu”amesema Fimbo.

Fimbo ametaja baadhi ya madhara ambayo mtu anaweza kupata endapo atatumia dawa za kuongeza mwili zenye madhara kwa binadamu, ametaja madhara hayo kuwa mwili kuongezeka na kuwa mkubwa sana, kupata shinikizo la damu, kisukari, moyo na mengine mengi.

Aidha TFDA iliamua kutoa tamko hilo mara baada ya dawa aina ya Advit DE+H inayoongeza vitamini A, D3, E na H kutangazwa mtandaoni kuwa unaongeza mwili na inauzwa kwa bei rahisi japo maelezo ya dawa hiyo yameelezwa ni maalumu kwa matumizi ya wanyama na si binadamu.

Aidha dawa za asili ambazo zimethibitishwa na TFDA ni ‘Ujana’ dawa nyingine zikiwa Sudhi, Vatari, IH Moon na Coloidal Silver ambazo kazi yake ni kukemea vimelea mbalimbali.

Moto wazuka wodi ya wazazi, vichanga matatani
Rais wa Ghana amsweka ndani Mwenyekiti wa Shirikisho la Kandanda

Comments

comments