Tuzo  ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara inatarajiwakufanyika Juni 23 mwaka huu ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Kufanyika kwa tuzo hizo ni utaratibu ambao Shirikisho la soka nchini Tanzania (TFF), limejiwekea kila mwaka baada ya kumalizika ligi kutoa tuzo kwa waliofanya vizuri kwa kushirikiana na Wadhamini wakuu wa VPL Kampuni ya Simu za mkononi ya Vodacom Plc na msimu huu tutakuwa na washirika wengine Azam Tv, Benki ya KCB na Premier Bet

Licha ya Tuzo ya Mchezaji Bora wa mwaka wa ligi, pia kunatolewa tuzo mbalimbali, ambapo kwa mwaka huu tuzo moja imeondolewa na nyingine imeongezwa ikiwa ni katika kuboresha.

Tuzo iliyoondolewa ni ya Mchezaji Bora wa Kigeni na imefanyika hivyo ili kuwapa fursa wachezaji wote kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora wa ligi kuu badala yakuwatenganisha.

Pia msimu huu imongezwa Tuzo ya Mwamuzi Bora Msaidizi ambayo haikuwepo msimu uliopita, hiyo ni kutokana kuthamini nafasi ya waamuzi wasaidizi.

Kwa mazingira hayo tuzo zitakazotolewa Juni 23, ambapo wadhamini wakuu ni Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom ni hizi zifuatazo:

Bingwa, Mshindi wa Pili, Mshindi wa Tatu, Mshindi wa Nne,  Mfungaji Bora, Timu yenye nidhamu, U20 Player (Tuzo ya Ismail Khalfan), Mchezaji Bora Chipukizi, Mwamuzi Bora Msaidizi, Mwamuzi Bora, Kipa Bora, Kocha Bora, Goli Bora  , VPL Best Eleven na Mchezaji wa heshima.

Zawadi kwa kila kipengele pamoja na majina ya wanaowania tuzo ukiacha bingwa, mshindi wa pili, wa tatu, wa nne na mfungaji bora ambao hujulikana kulingana na ligi inavyoendelea zitatangazwa siku za usoni.

Orodha ya wanaowania tuzo VPL 2017/18
Rooney kutimkia Marekani