Shirikisho la soka nchini (TFF) limezikumbusha timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwamba hazitopata leseni ya mchezaji yeyote ambaye timu haitapeleka mkataba wake wakati wa maombi ya usajili, hii ni kwa mujibu wa kanuni ya 68 vipengele vya 1, 2, 3 na 8 ya Ligi Kuu ya Tanzania toleo la 2016/2017.

TFF imeeleza kwamba kila timu inatakiwa kupeleka  nakala tatu za mkataba wa mchezaji, ili kamati ya katiba, sheria na hadhi za wachezaji iweze kupitia na TFF iweze kuidhinisha mikataba hiyo. Baada ya hapo timu na mchezaji, watakuja kuchukulia mikataba hiyo hapa TFF. Na kanuni ya 68(8) inataka kulipia kiasi cha sh 50,000 kwa kila mkataba wa mchezaji.
Kanuni hiyo hiyo imedhamiriwa kufuatwa ili kuondoa migogoro kati ya timu na mchezaji.
Kadhalika, kwa mujibu wa kanuni 67 vipengele vya 1, 2, 3 na 8 ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania ya StarTimes, Shirikisho la Mpira wa MiguuTanzania (TFF) linakumbusha kwamba halitatoa leseni ya mchezaji yeyote ambaye timu haikuleta mkataba wakati wa maombi ya usajili.
Hivyo kila timu imetakiwa kupeleka  nakala tatu za mkataba wa mchezaji, ili kamati ya katiba, sheria na hadhi za wachezaji iweze kupitia na TFF iweze kuidhinisha mikataba hiyo. Baada ya hapo timu na mchezaji watachukua mikataba hiyo katika ofisi za  TFF.
Kanuni ya 67(8) inazitaka klabu za ligi daraja la kwanza kulipia kiasi cha sh 25,000 kwa kila mkataba wa mchezaji.

Serikali Kuanza Kutoa Hati Miliki Na Upangaji Miji
FIFA Yaipa Heshima Tanzania Kupitia TFF