Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF limeburuzwa mahakamani na kampuni ya Smart Sports kwa madai ya kutoa hundi hewa kwa kampuni hiyo.

Kampuni ya Smart Sports imeishtakia TFF kwenye mahakama ya kisutu ikataka ilipwe Shilingi milioni 15 baada ya kuiuzia TFF vifaa vya mazoezi kwa timu za Taifa.

Katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, kesi ya hundi hewa inayolikabili shirikisho la soka Nchini imeanza kusikilizwa Alhamisi hii.

Kesi hiyo namba 175 ya 2016 imefunguliwa June 27 mwaka huu, ambapo Smart Sports imeilalamikia TFF kwa kuwapa hundi hewa.

Mwaka 2014 Smart Sports iliuzia TFF vifaa vya michezo pamoja na kutoa huduma ya usafiri kwa timu za Taifa, zenye thamani ya shilingi milioni 31.

February 23 TFF ikamkabidhi hundi Mkurugenzi wa Smart Sports Bwana GEORGE Wakuganda, lakini hundi hiyo ikashindikana kufanya malipo yaani imebaounce.

March 29 TFF ikakabidhi tena hundi kwa Wakuganda, na baada ya kwenda banki akakutana na hali ile ile.

Hapo ndipo Wakuganda akaanza harataki za kudai haki yake mahakamani.

March 29 Smart Sports ikawaandikia barua TFF kuulizia malipo hayo lakini TFF haikujibiwa.

June 15 2016 Smart Sports kupitia wakili wake akaindia barua TFF lakini TFF ikauchuna tena.

Kesi hiyo imesikilizwa Alhamisi hii kwa mara ya kwanza lakini TFF hawakutokea mahakamani licha kupekelekewa barua ya wito iliyowafikia  June 11 mwaka huu.

Nae mkurugenzi wa Smartsports amesema amemua kwenda mahakamani baaada ya kuona TFF hawataki kulipa deni kiungwana.

Kesi hiyo itasikilizwa tean August 3 mwaka huu..

Video: CCM iko pale pale na waliokuwa wanadhani wangeibuka hawakuibuka na hawataibuka - Kikwete
Mkwasa Kutangaza Kikosi Juma Lijalo