Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo matumizi ya fedha kiasi cha shilingi bilioni 3.7

Hayo yamesemwa hii leo jijini Dar es salaam na Rais wa Shirikisho hilo, Wallace Karia alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa fedha hizo zimetumika kwenye matumizi mbalimbali ya uendeshaji wa shughuli za mchezo wa soka nchini, ikiwemo Ligi mbalimbali nchini, vyama vya soka vya mikoa pamoja na malipo ya wafanyakazi na mafunzo mbalimbali.

Amesema ndani ya uongozi wake amefanikiwa kulipa deni la Bilioni 1.2 ambalo alilikuta TFF ikidaiwa na TRA, Mfuko wa Jamii (NSSF) pamoja na wafanyakazi na watoa huduma mbalimbali ndani ya shirikisho.

Kuhusu wafanyakazi kutopewa ajira Karia amesema ni kweli shirikisho limepunguza idadi ya wafanyakazi kutoka 44 mpaka 21, ambao wapo kwasasa huku wengine wakiwa wanajitolea na kufanya mafunzo kwa vitendo na endapo watafikia vigezo watapewa ajira za kudumu.

Hata hivyo, ameongeza kuwa moja ya mafanikio mengine ya uongozi ni kuingiza timu 4 za taifa za soka kambini kwa ajili ya michuano mbalimbali ndani ya mwezi April. Timu hizo ni Taifa Stars, Twiga Stars, Ngorongoro Heroes na Serengeti Boys.

 

 

JPM awashangaa wanaohoji viwanda
Mama Uwoya asema haitambui ndoa ya mwanae na Dogo Janja.