Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imefanya mabadiliko ya timu zilizo kwenye makundi ya ‘A’ na ‘B’ katika Ligi Daraja la Kwanza (FDL) Tanzania Bara iliyopangwa kuanza Septemba 16, mwaka huu.

Timu zilizofanyiwa mabadiliko ni Polisi Morogoro FC ya Morogoro iliyokuwa kundi ‘A’ sasa itakuwa Kundi ‘B’ wakati Mshikamano FC ya Dar es Salaam iliyokuwa Kundi ‘B’ sasa itacheza mechi zake katika Kundi ‘A’.

Makundi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kwa timu 24 zilizogawanywa katika makundi matatu yenye timu nane kila kundi zitakazochuana msimu huu wa 2017/18 kuwania nafasi tatu muhimu za kupanda daraja kucheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu wa 2018/19.

Taarifa iliyotolewa na TFF ya marekebisho hayo ni kwamba Kundi ‘A’ litakuwa na timu za African Lyon, Ashati United, Friends Rangers, Mshikamano za Dar es Salaam, JKT Ruvu na Kiluvya United za Pwani, Mgambo JKT ya Tanga na Mvuvumwa ya Kigoma.

Kundi ‘B’ zitakuwa timu za Coastal Union ya Tanga, JKT Mlale ya Ruvuma, KMC ya Dar es Salaam, Mbeya Kwanza ya Mbeya, Mufindi United ya Iringa, Polisi Dar za Dar es Salaam na Polisi Morogoro na Mawenzi Market ya Morogoro.

Hata hivyo, Kundi ‘C’ litakuwa na timu za  Alliance School, Pamba na Toto African za Mwanza, Rihno Rangers ya Tabora, Polisi Mara ya Mara, Polisi Dodoma ya Dodoma, Transit Camp ya Shinyanga na JKT Oljoro ya Arusha.

Picha: Wafuasi wa Lipumba na Maalim Seif wanyukana mahakamani
Ben Pol: Hakuna kilichotengenezwa ni maisha yangu halisi na Ebitoke