Klabu ya Yanga imetozwa faini ya Tsh. 3,000,000 (milioni tatu) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutokana na wachezaji wa timu hiyo kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi katika mechi dhidi ya Namungo FC iliyofanyika Aprili 4, 2019 katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara huku ikielezwa kuwa hilo ni kosa la nne msimu huu kwa wachezaji wa Yanga kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi, na adhabu dhidi yake imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 14 (49) ya Ligi Kuu Toleo la 2018 kuhusu Taratibu za Mchezo.

Yanga pia imetozwa faini ya Tsh. 500,000 (laki tano) kutokana na mashabiki wake kuwarushia chupa za maji waamuzi wakati wakirejea vyumbani baada ya mechi hiyo kumalizika. adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni ya 43(1) ya Ligi Kuu Toleo la 2018 kuhusu Udhibiti kwa Klabu.

Aidha, mchezaji Kelvin Yondani wa Yanga amefungiwa mechi tatu na kutozwa faini ya Tsh. 500,000 (laki tano) baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumpiga ngumi mchezaji wa Kagera Sugar FC katika mechi hiyo iliyochezwa Aprili 11, 2019 kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Mchezaji Paul Peter wa Azam FC amefungiwa mechi tatu na kutozwa faini ya Tsh. 500,000 (laki tano) baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumpiga ngumi mchezaji wa Mbeya City FC katika mechi hiyo iliyochezwa Aprili 14, 2019 kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya. adhabu hiyo ni uzingativu wa Kanuni ya 38(9) ya Ligi Kuu Toleo la 2018 kuhusu Udhibiti kwa Wachezaji.

Aidha, mchezaji, Aggrey Morris wa Azam FC amefungiwa mechi tatu na kutozwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) baada ya kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kosa la kumpiga ngumi mchezaji wa Mbao FC katika mechi hiyo ya Aprili7, 2019 iliyochezwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Imeelezwa kuwa, adhabu hizo ni uzingativu wa Kanuni ya 38(9) ya Ligi Kuu Toleo la 2018 kuhusu Udhibiti kwa Wachezaji.

Namungo FC imepewa ushindi wa pointi tatu na mabao matatu baada ya Friends Rangers FC kugomea mchezo huo uliofanyika Aprili 13, 2019 kwenye Uwanja wa Majaliwa ulioko Ruangwa mkoani Lindi, hadi mchezo huo unavunjwa na Mwamuzi kutokana na timu ya Friends Rangers kutoka uwanjani, Namungo FC ilikuwa ikiongoza mabao 2-0.

Kwa upande wa Klabu ya Ndanda SC imetozwa faini ya sh. 1,500,000 (milioni moja na nusu) kwa kosa hilo hilo. Hilo ni kosa la kwanza msimu huu kwa timu ya Ndanda SC kuingia uwanjani kwa kutumia mlango usio rasmi. Adhabu dhidi ya Ndanda pia ni kwa mujibu wa Kanuni ya 14(49) ya Ligi Kuu Toleo la 2018 kuhusu Taratibu za Mchezo.

Wagonjwa 15 wafanyiwa upasuaji
Video: Serikali yataka kila mtanzania kumiliki laini moja ya simu

Comments

comments