Shirikisho la soka nchini TFF limekanusha taarifa inayoendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, ikidai shirikisho hilo limeifuta sheria namba 11 katika michezo yote itakayowahusisha mabingwa wa soka Tanzania bara Simba SC.

Taarifa hiyo ilianza kusambazwa dakika chache baada ya mchezo wa Simba SC na Polisi Tanzania kumalizika uwanja wa Taifa jana usiku, huku wenyeji wakibuka na ushindi wa mabao mabao mawili kwa moja.

Chanzo cha kuibuliwa kwa taarifa hizo zilizokanushwa na TFF, ni kufuatia malalamiko ya baadhi ya mashabiki kudai mfungaji wa bao la kusawazisha na Simba SC John Bocco, alikua ameotea kabla ya kukwamisha mpira kwenye lango la Polisi Tanzania ambao walikua wanaongoza.

Utata wa mabao ya kuotea umekua gumzo miongoni mwa mashabiki wa soka nchini Tanzania wanaofuatilia ligi kuu, huku klabu ya Simba SC ikitajwa kuhusishwa kwenye utata huo mara kwa mara.

Wakati huo huo ligi kuu ya soka tanzania bara itaendelea tena hii leo kwa michezo kadhaa kuchezwa katika viwanja tofauti.

Mchezaji wa Uganda afungiwa maisha
Spika achana hotuba ya Rais