Shirikisho la soka nchini TFF, limekanusha taarifa za kuvuja kwa ratiba ya ligi ya soka Tanzania bara msimu wa 2016/2017, ambayo ilisambazwa katika mitandao ya kijamii mapema hii leo.

Taarifa iliyotolewa na idara ya habari na mawasilino ya shirikisho hilo, imeeleza kwamba ratiba inayodaiwa kuvuja ina mapungufu mengi ambayo inaonyesha dhahir haikuwa sahihi.

“Ile ya mitandao ya kijamii imekosewa anwani ya Posta ya TFF kadhalika kuonesha kuwa mchezo kati ya Azam FC na African Lyon ungefanyika Agosti 21, 2016 ilihali hii rasmi ina anwani sahihi na mchezo huo wa raundi ya kwanza ukionesha utachezwa Agosti 20, 2016.” Imeeleza taarifa ya TFF iliyosambwazwa katika vyombo vya habari.

Katika hatua nyingine shirikisho la soka nchini TFF, limetangaza rasmi ratiba ya msimu wa 2016-17 ambayo inaonyesha michezo ya ligi hiyo itaanza kuunguruma Agosti 20 katika viwanja mbalimbali nchini kote.

“Ratiba hiyo imezingatia michuano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa kwa ngazi ya klabu na timu za taifa ili kukwepa dhana yoyote ya upangaji wa matokeo na kurundikana kwa michezo.” Imesisitiza taarifa ya TFF

Hata hivyo TFF imeiomba familia ya soka kuegemea kwenye ratiba ioliyotolewa muda mchache uliopita, ambayo inaonyesha mabingwa watetezi Young Africans hawatocheza mchezo wao wa ufunguzi ambao ungewakutanisha na JKT Ruvu, hivyo mchezo huo umehamishwa na kuepelekwa Agosti 31.

Young Africans wataanza kibarua chao cha kutetezi ubingwa kwa kucheza dhidi ya African Lyon Agosti 28.

Michezo mingine ya ufunguzi ambayo itachezwa Agosti  20, Wekundu wa Msimbazi Simba wataanza kupambana na Ndanda FC.

Kagera Sugar Vs Mbeya City

Toto Africans Vs Mwadui FC

Stand Utd Vs Mbao FC

Mtibwa Vs Ruvu Shooting

Azam FC Vs African Lyon

Majimaji FC Vs Tanzania Prisons

Ratiba hiyo inaonyesha mahasimu katika soka la Tanzania, Young Africans na Simba SC watakutana Oktoba mosi katika uwanja wa taifa ambapo mabingwa watetezi watakua wenyeji.

Na mchezo wa mkondo wa pili kwa wawili hao umepangwa kufanyika Februari tano mwaka 2017, ambapo Simba watakuwa wenyeji.

Wanafunzi Watakao hakikiwa vyuo Vikuu kupata Fedha za mafunzo
Kiwanda Cha Pepsi Cha Jijini Dar Es Salaam Chapigwa Faini