Shirikisho la soka nchini TFF limekemea vitendo vya vurugu vinavyofanya na baadhi ya Mashabiki katika michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara, ambayo imeingia kwenye mzunguuko watano.

TFF imetoa taarifa ya kukemea vitendo hivyo na kuisambaza kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii, huku ikiwakumbusha Mashabiki wanaofika viwanjani, kujenga utamaduni wa kuwa na vitendo vya kiungwana (Fair Play).

Hata hivyo TFF haijafafanua michezo iliyowasukuma kutoa taarifa hiyo ya kukemea vurugu, huku ikisisitiza kuendelea kufuatilia kwa ukaribu watakaokiuka agizo hilo, na kuahidi kuwachukulia hatua za kinidhamu itakapobidi.

May be an image of text

Nani kasema Diamond Platnums ni mtu mbaya?
Azam FC: Lwandamiza hajafukuzwa, hafukuzwi